Haki Yako ya Kupata Huduma za Lugha
Una haki ya kufikia mipango, misaada na huduma za jimbo katika lugha yako mwenyewe, bila malipo. Unaweza kupata huduma za ukalimani na pia kutafsiriwa hati muhimu katika lugha unayoitumia unapowasiliana na Idara ya Watoto, Vijana na Familia (Department of Children, Youth, and Families, DCYF), kuomba misaada au huduma za jimbo, au kuhudhuria mafunzo au hafla.
Pata Huduma za Lugha
Kupata huduma za lugha, tafadhali shirikiana moja kwa moja na mwakilishi wako wa DCYF au utume barua pepe kwa idara ya Huduma za Ufikiaji wa Lugha kupitia dcyf.languageaccess@dcyf.wa.gov.
Nyenzo Nyinginezo za Kukusaidia
Ripoti Unyanyasaji au Kutekelezwa kwa Mtoto
1-866-363-4276
Kuripoti unyanyasaji au kutelekezwa kwa mtoto, watunzaji wa watoto wasio na leseni na masuala mengine yanayohusiana na watoto. Opereta anaweza kukuunganisha na mkalimani anayezungumza lugha yako.
Idara ya Mahusiano ya Wadau
ConstRelations@dcyf.wa.gov | 1-800-723-4831 | 360-902-8060
Idara ya Mahusiano ya Wadau inatoa mchakato wa haki na wenye heshima wa kusuluhisha malalamiko kuhusu ulinzi wa watoto na masuala ya masilahi ya watoto, utoaji wa leseni za makazi ya malezi na za utunzaji wa watoto, mipango ya utunzaji wa watoto na huduma za urekebishaji wa watoto.
Nambari Kuu ya Huduma za DCYF
1-866-363-4276
DCYF ina nyenzo nyingi kwa ajili ya familia. Unaweza kupata baadhi ya hizo kwa kupiga nambari kuu ya huduma bila kulipishwa. Opereta anaweza kukuunganisha na mkalimani anayezungumza lugha yako.
Huduma zinazopatikana ni pamoja na:
- Huduma za usaidizi wa mapema kwa watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 3.
- Mipango ya jimbo zima ya usaidizi, elimu na uongozi.
- Usaidizi wa kupata huduma salama na nafuu za utunzaji wa watoto.
- Mipango ya kutembelewa nyumbani, mahusiano ya jamii na ufadhili.
- Uelekezaji kwa huduma na usaidizi wa kijamii katika eneo la karibu.
Tuma Malalamiko kuhusu Ubaguzi
Tafadhali jaza Fomu ya DCYF ya Malalamiko Kuhusu Ufikiaji wa Huduma na Haki za Raia kwa malalamiko yanayohusiana na Sheria ya Wamarekani wenye Ulemavu (Americans with Disabilities Act), Sehemu ya 504 ya Sheria ya Urekebishaji (Rehabilitation Act), Toleo la VI la Sheria ya Haki za Raia (Civil Rights Act), Ufikiaji wa Lugha na Ubaguzi wa Vikundi Vinavyolindwa.